Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Felix Tshisekedi kurejea nchini kuzindua kampeni zake za uchaguzi

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi anatarajiwa kurejea katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa ili kuzindua kampeni zake akigombea nafasi ya urais.

Félix Tshisekedi (kushoto) na Vital Kamerhe (kulia).
Félix Tshisekedi (kushoto) na Vital Kamerhe (kulia). Photo-Montage/RFI/© AFP
Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi ataingia kwenye kinyang'anyiro ca urais na mwenziwe Vital Kamerhe kama mgombea mwenza.

Felix Tshisekedi, ambaye ni kiongozi wa chama kikongwe cha upinzani nchini DRC, UDPS, pamoja na Vital Kamerhe, wa chama cha UNC, wanatarajiwa kuzindua kampeni zao kwa pamoja, baada ya makubaliano ya kuunganisha nguvu.

Hata hivyo wadadisi wanasema hali hiyo itasababisha upinzani unapoteza nguvu yao kwa kugawana kura wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Hivi karibuni Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe waliondoa saini zao kwenye makubaliano ya kumteua Martin Fayulu kama mgombea mmoja wa upinzanim, hali ambayo ilizua sintofahamu kwa upande wa upinzani ikiwa imesalia siku zisizozidi thelathini kabla ya Uchaguzi wa urais nchini humo.

Tshisekedi sasa atawania nafasi ya urais kwa makubaliano kwamba Kamerhe atakuwa waziri mkuu wake ikiwa watashinda uchaguzi.

Felix Tshisekedi ni mtoto wa Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mwaka uliyopita baada ya kutumikia miongo kadhaa kambi ya upinzani nchini DRC.

Wagombea 19 kwa ujumla wanawania nafasi moja ya urais ikiwa ni pamoja na mgombea wa muungano wa vyama vinavyoshiriki serikalini, Emmanuel Ramazani Shadary.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.