Pata taarifa kuu
DUNIA-HAKI YA MTOTO

Dunia yaadhimisha siku ya kimataifa ya haki za mtoto

Dunia inaadhimisha siku ya Kimataifa ya watoto hivi leo. Umoja wa Mataifa unasema siku hii imetengwa mahsusi kuikumbusha dunia kuwa, watoto wana haki ambazo hazistahili kupuuzwa.

Kwa mujibu wa UNICEF, mamilioni ya watoto wako katika hatari ya kukabiliwa na ghasia na ukatili.
Kwa mujibu wa UNICEF, mamilioni ya watoto wako katika hatari ya kukabiliwa na ghasia na ukatili. RFI/Florence Morice
Matangazo ya kibiashara

Haki muhimu kwa watoto kupata malezi bora na kwenda Shule na kupinga ukatili ili wawezeke kufikia malengo yao.

Hata hivyo, haki za watoto hao zimeendelea kukiukwa hasa katika mataifa ya Afrika, hasa katika nchi ambazo zinashudia vita kama Somalia, Sudan Kusini, Mashariki mwa DRC na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Siku ya Kimataifa ya Watoto Duniani, iliotengwa maalumu ili kuikumbusha jamii juu ya haki na ustawi wa watoto. Kulingana na ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Kulinda Watoto Save the Children ,zaidi ya nusu ya idadi nzima ya watoto duniani wanakabiliwa na vitisho vya migogoro, umasikini na ubaguzi katika jamii zao.

UNICEF inasema wakati hatua zimepigwa katika kupunguza vifo vya watoto na kuboresha afya duniani kote, mamilioni ya watoto wako katika hatari ya kukabiliwa na ghasia na ukatili.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF Athony Lake amesema msukumo wa siku ya kimataifa ya haki za watoto mwaka huu ni ndoa za utotoni ambazo zinaathiri wasichana wengi.

Amesema wasichana hao wanaoolewa wakiwa wadogo sana wanakuwa katika hatari ya kunyanyaswa, kutendewa ukatili na pia wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kuliko wanawake waliopevuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.