Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Kampeni za uchaguzi kuanza Alhamisi DRC

Kampeni za uchaguzi nchini DRC zinaanza Alhamisi wiki hii, wakati huu wanasiasa wanaoishi nje ya nchi hiyo walioruhusiwa kushiriki katika Uchaguzi wa tarehe 23 mwezi Desemba, wakitarajiwa kurejea nyumbani.

Maandamano dhidi ya mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 23 DRC, Oktoba 26, 2018  Kinshasa.
Maandamano dhidi ya mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 23 DRC, Oktoba 26, 2018 Kinshasa. AFP/Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

Kampeni hii muhimu, inakuja wakati huu wanasiasa wa upinzani wakiwa wamegawanyika, kuelekea Uchaguzi huo, huku muungano wa vyama tawala FCC vikimalizia mikutano ya kuwaandaa watu 500 watakaozunguka nchi hiyo kumtafutia kura mgombea wao Emmanuel Ramazani Shadary.

Mgombea wa upinzani Martin Fayulu, aliyeteuliwa na wenzake kuwania urais katika Uchaguzi huo, naye anatarajiwa kurejea nyumbani siku ya Jumatano.

Hata hivyo, wanasiasa wawili felix Tshisekedi, wa UDPS, vital Kamerhe wa UNC tayari wamejiondoa kwenye mkataba wa kumuunga mkono Bwana Fayulu, baada ya shinikizo kutoka kwa wafuasi wao na kuacha upinzani uliogawanyika.

Kampeni ya mwezi mzima, inaanza wiki hii, wakati huu mvutano ukiendelea kuhusu matumizi ya mashine za kuwatambua wapiga kura.

Tume ya Uchaguzi CENI inasema, mashini hizo zitatumika lakini wanasiasa wa upinzani wanapinga, na kusema kuwa wana wasiwasi kuwa zitatumiwa kuiba kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.