Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Wanafunzi wawili wafariki kutokana na majeraha ya risasi DRC

Wanafunzi wawili walifariki dunia wiki hii baada ya kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano katika Chuo Kikuu cha Kinshasa, nchini DRC, polisi imesema leo Ijumaa.

Magari ya serikali yaliyochomwa na wanafunzi wa kitivo cha Ujenzi (INBTP) wakati wa maandamano katika makabiliano na polisi, Kinshasa, DRC.
Magari ya serikali yaliyochomwa na wanafunzi wa kitivo cha Ujenzi (INBTP) wakati wa maandamano katika makabiliano na polisi, Kinshasa, DRC. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

"Wanafunzi wawili walipoteza maisha kutokana na majeraha ya risasi" wakati wa maandamano dhidi ya mgomo wa walimu, Jenerali Sylvano Kasongo, mkuu wa polisi wa katika mji mkuu wa DRC ameandika katika taarifa.

Tangu Jumatatu, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kinshasa (Unikin) wanaandamana wakidai mgomo wa walimu ulioanza miezi miwili iliyopita, usitishwe.

Hayo ya kijiri polisi ilifaulu kuzima maandamano mengine mapema Ijumaa asubuhi, kwa mujibu wa mwanafunzi, waliohojiwa na AFP.

"Polisi inawatolewa wito wanafunzi kuwa watulivu na kuwahakikishiakwamba hatua zote zimechukuliwa ili kuwakamata waliohusika na kitendo cha kuwafyatulia risasi wanafunzi hao wawili na wahukumiwe kwa mujibu wa sheria," Jenerali Kasongo amebaini.

Kwa mujibu wa Jenerali Kasongo, "polisi aliyefyatulia risasi wanafunzi wawili siku ya Jumatatu alikamatwa na atafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi".

Shirika la haki za binadamu nchini DRC, ACAJ, limesema lina wasiwasi kuhusu "ukandamizaji wa kikatili dhidi ya maandamano ya wanafunzi, kitendo ambacho kkinaendeshwa na polisi". ACAJ imelaani kitendo hicho na kusikitishwa na vifo vya wanafunzi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.