Mfalme Mohammed VI pamoja na Maaskofu Katoliki nchini Morocco, wamemwalika Baba Mtakatifu Francisko kutembelea nchi yao kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019. Katika ziara hii, Papa Francis anatarajiwa kutembelea mji wa Rabar na Casablanca.
Ratiba ya ziara hii inatarajiwa kutolewa hivi karibuni kwa mujibu wa Dr. Greg Burke, msemaji mkuu wa Vatican.
Papa Francis anataka kuendeleza majadiliano ya kidini na waamini wa dini mbali mbali duniani, ili kujenga na kudumisha umoja, upendo, haki na mshikamano wa dhati na kwamba, tofauti mbali mbali zisiwe ni chanzo cha vurugu na mitafaruku ya kijamii na kidini, Dr. Greg Burke amesema.
Papa Francis ni kiongozi wa pili wa kanisa Katoliki kuzuru Morocco baada ya Papa John Paul II kuzuru nchi hiyo mnamo mwaka 1985 wakati wa utawala wa Hassan II.