Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Rais anaye maliza muda wake Madagascar atishia kutokubali matokeo ya uchaguzi

Rais wa zamani wa Madagascan, Hery Rajaonarimampianina, amedai kuwa chama chake kimegundua kuwepo kwa dosari nyingi za uchaguzi katika uchaguzi uliofanyika juma hili, matamshi yanayozusha wasiwasi wa kuzuka kwa maandamano na kupingwa kwa matokeo.

Hery Rajaonarimampianina (picha ya kumbukumbu).
Hery Rajaonarimampianina (picha ya kumbukumbu). RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali kutoka katika baadhi ya vituo yanamuweka rais Hery katika nafasi ya tatu nyuma ya wagombea wengine Andry Rajoelina na Marc Ravalamonana ambao wote waliwahi kuwa viongozi wa taifa hilo kwa nyakati tofauti.

Rais Rajaonarimampianina akizungumza mjini Antananarivo, amesema uchaguzi huo ulikuwa na dosari za kiufundi ikiwemo orodha ya watu waliosajiliwa kimakosa, vitisho na uwepo wa karatasi ambazo tayari zilikuwa zimepigwa kura.

Kwenye taarifa yake kiongozi huyo amesema hawatakubali kuona wananchi wananyang’anywa haki kupitia kura waliyopiga.

Hata hivyo matamshi ya Rais Rajaonarimampianina yanakinzana na yale ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ambao waliotoa taarifa za awali kueleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na hapakuwa na dosari kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.