Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Mkuu kufanyika mwezi Mei 2019 Afrika Kusini

Mamlaka nchini Afrika Kusini zimetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika Mwezi Mei mwaka 2019. Utakuwa ni uchaguzi utakaopima umaarufu wa rais Cyril Ramaphosa na chama tawala cha ANC amabcho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1994.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Julai 27, 2018.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Julai 27, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tarehe hiyo imetangazwa wakati huu Rais Cyril Ramaphosa na chama tawala cha ANC wakijaribu kuwashawishi wafuasi wa chama hicho kuwaunga mkono ili kubadili taswira waliyonayo wananchi kuhusu chama hicho kushindwa kutatua changamoto za kiuchumi.

Chama cha ANC kinatarajiwa kupata ushindani mkubwa kutoka chama cha upinzani Democratic Alliance na kile cha Economic Freedom Fighters.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance na kile cha Economic Freedom Fighters vyenyewe vinajaribu kuingia katika uchaguzi huo vikiwa na imani kuwa wataweza kuwashawishi wananchi kuwaamini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.