Rais wa Cameroon Paul Biya kwa mara ya kwanza amekiri kukabiliwa na changamoto ya kurejesha imani na utulivu kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ambako raia wake wanazungumza lugha ya Kiingereza.
Akizungumza wakati wa kuapishwa kwake siku ya Jumanne, Rais Biya amewaonya waasi wa eneo hilo wanaoendesha vitendo vya kihalifu, akiipa Serikali yake kushughulikia mzozo wa eneo hilo akiwataka waasi hao kuweka silaha chini ama wakabiliwe na nguvu ya vyombo vya sheria.
Siku ya Jumanne jioni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress alitoa wito wa kuachiliwa huru kwa wanafunzi hao..
Maeneo ya Kaskazini-Magharibi yanaendelea kukumbwa na machafuko, baada ya wanaharakati kutaka maeneo hayo kuwa taifa huru la Ambazonia.
Hakuna taarifa zaidi kuhusu waalimu watatu ambao walikuwa wameongozana na watoto wao.