Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Upinzani DRC kumteua mgombea mmoja Uswisi

Vigogo saba wa upinzani nchini DRC wanatarajia kuteua mgombea mmoja kuelekea uchaguzi wa urais wa Desemba 23 katika mkutano utakaofanyika siku ya Alhamisi huko Geneva, nchini Uswisi, licha ya ya mvutano unaoendelea katika kambi hiyo.

Kutoka kushoto kwenda kulia, , viongozi wa upinzani wa DRC Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Adolphe Muzito, Moise Katumbi na Jean-Pierre Bemba, katika mkutano wa Brussels mnamo 4 Septemba 2018.
Kutoka kushoto kwenda kulia, , viongozi wa upinzani wa DRC Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Adolphe Muzito, Moise Katumbi na Jean-Pierre Bemba, katika mkutano wa Brussels mnamo 4 Septemba 2018. © AFP/John Thys
Matangazo ya kibiashara

"Hadi tarehe itakayotangazwa, viongozi wote wa upinzani watakutana nchini Uswisi kushiriki katika mkutano wa kuteua mgombea mmoja wa upinzani atakayepeperusha bendera ya upinzani katika ucaguzi wa urais " wa Desemba 23, Freddy Matungulu, mmoja wa wagombea wanne wa upinzani ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mnamo Oktoba 26 huko Afrika Kusini, vigogo saba wa upinzani waliahidi kuteua mgombea mmoja kabla ya Novemba 15 kwa ajili ya uchaguzi utakaopelekea kupatikana kwa mrithi wa Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani kwa miaka miaka 18.

"Matarajio ni makubwa kutoka kwa raia, na kama kundi tunategemea ushindi katika uchaguzi wa urais tukiwa pamoja," amesema Matungulu.

"Mkutano wa Uswisi unaweza kuchukua siku tatu," Wakili Peter AFP Kazadi, Naibu mkurugenzi wa wagombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha upinzani cha kihistoria (UDPS ). "Rais Tshisekedi atakuwepo," Kazadi alisema.

Mkutano huu umepangwa kwa tofauti za msingi juu ya matumizi ya mashine za kupiga kura ambazo zinapaswa kuruhusu wapigakura kuchagua mgombea wao na magazeti kura katika vituo vya kupigia kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.