Pata taarifa kuu
MISRI-IS-USALAMA

Wanajihadi 19 wauawa Misri

Wanajihadi 19 waliokuwa wamehusishwa na tukio la kigaidi la kuwashambulia wakiristo saba wa dhehebu la Coptic nchini Misri, wameuawa.

Kanisa kuu la Wakristo wa dhehebu la Coptic la Assouan, Misri.
Kanisa kuu la Wakristo wa dhehebu la Coptic la Assouan, Misri. Michel Benoist/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema, washukuwa hao waliuawa katika makabiliano makali na maafisa wa usalama. Shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa (Desemba 29)

Misri imeendelea kusumbuliwa na makundi ya kigaidi, huku Wakiristo wa dhebu la Coptic wakiwa hatarini.

Siku ya Ijumaa watu wasiopungua saba waliuawa katika shambulio dhidi ya kanisa la Coptic kusini mwa Cairo, nchini Misri.

Shambulizi hili linathibitishwa kuwa waumini wa Kanisa la Coptic bado wanaendelea kulengwa na Waislamu wenye msimamo mkali. Makanisa matatu yamelengwa tangu mwezi Desemba 2016. Wakristo 100 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.