Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Mzozo waibuka baada ya kutangazwa kwa timu ya kampeni ya Emmanuel Shadary

Baadhi ya wajumbe walioteuliwa katika kamati ya watu 500 watakaomsaidia mgombea wa chama tawala nchini DRC Emmanuel Ramazani Shadary, kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 23 mwezi Desemba, wametupilia mbali uteuzi Wao.

Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC.
Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wanasema hawakupewa taarifa yoyote kabla ya hatua hiyo kuchukuliwa.

Miongoni mwao ni pamoja na Florent Ibenge, kocha wa timu ya taifa ya DRC Pamoja na Kasonga Tshilunde mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari nchini humo, UNPC ambaye amesema amestushwa na uteuzi wake.

Kamati hiyo inaundwa na Mawaziri na kuongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala, lengo likiwa ni kumsaidia mgombea wao kupata uungwaji mkono na kupigiwa kura wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Miongoni mwa Mawaziri waliopewa jukumu nzito katika Kamati hiyo ni Waziri wa Habari Lambert Mende ambaye atakuwa msemaji katika kampeni hiyo.

Kamati hiyo inatarajiwa kuzunguka nchi hiyo nzima, kufanya kampeni ili kuhakikisha kuwa Shadari anamrithi rais Joseph Kabila.

Shadary anayepewa nafasi ya kumrithi rais Kabila, amewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kumzuia kusafiri kwenda katika bara hilo kutokana na tuhma za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo, akiwa Waziri wa Mambo ya ndani.

Hata hivyo, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe, ambao haijafahamika iwapo wataungana kuelekea uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.