Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-RFI-HAKI

Mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon: Uchunguzi waendelea kusubiriwa

Manmo Novemba 2, 2013, wanahabari wenzetu wa RFI Ghislaine Dupont, na Claude Verlon, ambao walikuwa kikazi katika mji wa Kidal kaskazini mwa Mali walitekwa na kuuawa na watu waliowateka nyara. Miaka mitano baadaye, hakuna mwanga ambao umekwisha tolewa kuhusu mazingira ya mauaji yao na sababu za kutekwa nyara.

Claude Verlon na Ghislaine Dupont waliuawa tarehe 2 Novemba 2013.
Claude Verlon na Ghislaine Dupont waliuawa tarehe 2 Novemba 2013. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa uchunguzi unaendelea nchini Mali ambako kulitokea mauaji hayo na nchini Ufaransa. Uchunguzi huo unaendeshwa na Jaji Jean-Marc Herbaut.

Shahidi wa mwishoalisikilizwa mjini Paris mwezi mmoja uliopita, ishara kwamba uchunguzi unaendelea vizuri. Lakini zoezi la kuwasikiliza mashahidi linaendeshwa kwa mwendo wa kinyonga. "Hali hiyo inachosha," amesema mmoja wa mawakili, ambaye hata hivyo, kama wenzake wote amekaribisha ziara ya Jaji Herbaut katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mapema mwezi Februari.

Mwaka huu, hatimaye tumliweza kupata kitu ambacho tumekuwa tukidai kwa muda mrefu, ni kusema kwamba, majaji wawili kati ya majaji wanaoendesha uchunguzi walifanya ziara nchini Mali, walikutana na mwenzao kutoka Mali, na kumfahamisha kuhusu masuala wanayojiuliza, kwa mujibu wa wakili Caty Richard, mwanasheria wa Apolline Verlon, binti ya Claude Verlon

Jaji Herbaut alikutana kwa mara ya kwanza na mwenzake kutoka Mali ambaye anasema alifanya kazi naye usiku na mchana kwa muda wa siku kadhaa. Ziara hii imepelekea Jaji wa kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi kupata sehemu ya vitu walivyokuwa wakidai, lakini namba za simu zilizopatikana kwenye eneo la tukio hazikuzaa matunda yoyote.

Hata uchunguzi kwenye kompyuta ya Ghislaine Dupont haukuzaa matunda yoyote.

Miaka mitano baadaye,masuala muhimu bado yamesalia gizani, hasa kuhusu uhusiano wa kuachiliwa huru mateka wa Arlit zoezi lililotokea siku nne kabla.

"Kuhusu wahusika [wa kisa hiki cha utekaji nyara na mauaji], nadhani bado kuna majibu kutoka faili hii lakini kwa nini, linabakia kuwa swali na hadi sasa hatuna jibu lililotokana na faili hiyo. Hivyo basi inabidi uchunguzi uendelee, " wakili Valérie Courtois, mwanasheria wa Marie-Solange Poinsot, mama wa Ghislaine Dupont, amesema.

Uchunguzi upande wa Mali umesitishwa licha ya uteuzi wa jaji anayehusika na uchunguzi mwaka 2017.

Kulingana na taarifa ya RFI, bata hivyo, hakuna waranti wa kimataifa wa kukamatwa uliotolewa dhidi ya mmoja wa watuhumiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.