Pata taarifa kuu
DRC-UNSC-EBOLA-AFYA

Umoja wa Mataifa waamua kuweka nguvu pamoja dhidi ya Ebola DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne (Oktoba 30) lilipitisha kwa kauli moja azimio linalotaka kuimarisha uwezo zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola mashariki mwa DRC.

Wauguzi wakijiweka tayari kwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola katika kituo cha matibabu cha Ebola (CTE) huko Mangina, Kivu Kaskazini.
Wauguzi wakijiweka tayari kwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola katika kituo cha matibabu cha Ebola (CTE) huko Mangina, Kivu Kaskazini. Photo: Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wiki chache kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mnamo Desemba 23, Umoja wa Mataifa umeyataka makundi ya watu wenye silaha kusitisha shughuli zao ili kuruhusu msaada wakibinadamu na huduma za kiafya kuwafikia raia katika maeneo yanayoathiriwa naugonjwa wa Ebola. Azimio hilo pia linnasisitiza haja ya Monusco na shirika la Afya Duniani (WHO) kuratibu shughuli hizo kwa ushirikiano na serikali ya Congo.

Nakala hiyo, iliyowasilishwa na Ethiopia na Sweden, na kufadhiliwa na wanachama wote wa Baraza la Usalama, linahoji juu ya kikwazo kilichowekwa kwa wafanyakazi wa huduma za afya kwa kuwasaidia raia. Katika eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, shughuli za afya zilisimamishwa kwa ukosefu wa usalama wa kutosha, kwa mujibu wa balozi wa Ethiopia.

Wanadiplomasia wametoa wito kwa makundi yote ya waasi, na hasa kundi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Forces (ADF), kusitisha shughuli zao ili kuwezesha haraka utoaji wa misaada na usiozuilika. Hospitali na wahudumu una hofu kuwa kukosekana kwa huduma za afya, janga hilo linaweza kusambaa hadi katika nchi nyingine za ukanda huo kama vile Burundi, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.