Pata taarifa kuu
AU-KENYA-ODINGA

Mjumbe mpya wa Umoja wa Afrika kuhakikisha miradi ya barabara na reli zinakamilika

Mjumbe wa Umoja wa Afrika anayehusika na miundo mbinu ambaye pia ni kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema  atahakikisha kuwa anatumia nafasi hiyo kuona kuwa miradi ya reli na barabara inatekelezwa.

Mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga (Kulia) akiwa na Mkuu wa Tume ya Umoja huo Moussa Faki, wakiwa jijini Addis Ababa Oktoba 18 2018
Mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga (Kulia) akiwa na Mkuu wa Tume ya Umoja huo Moussa Faki, wakiwa jijini Addis Ababa Oktoba 18 2018 twitter.com/RailaOdinga
Matangazo ya kibiashara

Mwaka wa 1971, Umoja wa Afrika ulikuja na mpango wa kuliunganisha bara la Afrika kwa kutumia barabara na reli, kwa lengo la kuimarisha biashara na kuwawezesha waafrika kusafiri kwa urahisi.

Umoja wa Afrika unaamini kuwa kuwa na miundo mbinu imara, itasaidia pia katika vita dhidi ya umasikini.

Mradi huo ambao umekuwa ukitekelezwa polepole, unalenga kujenga barabara yenye urefu wa Kilomita 60,000 kati ya jiji la Cairo nchini Misri na Dakar, Senegal.

Barabara nyingine itatoka Cairo kwenda Cape Town Afrika Kusini na nyingine itatokea mjini wa Pwani wa Lagos kwenda mji mwingine wa Pwani wa Mombasa nchini Kenya.

Barabara pekee iliyokamilika ni ile kutoka Dakar kwenda N’Djamena nchini Chad yenye urefu wa Kilomita 4500.

Odinga atakuwa na Ofisi jijini Nairobi, Addis Ababa na Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.