Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Mji wa Oïcha wakumbwa na jinamizi la mauaji

Mji mkuu wa eneo la Beni, Mashariki mwa DRC, umeshambuliwa na watu wenye silaha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine wengi hawajulikani waliko. Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumatano kuamkia leo Ahamisi.

Tangu mwanzo wa mauaji Oktoba 2014 katika eneo la Beni, watu wengi walilazimika kutoroka makazi yao.
Tangu mwanzo wa mauaji Oktoba 2014 katika eneo la Beni, watu wengi walilazimika kutoroka makazi yao. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa mapema asubuhi na serikali katika eneo hilo, huku ikibaini kwamba nyumba saba zilichomwa moto na maduka kadhaa yaliporwa. Jeshi halijathibitisha idadi hiyo ya vifo. Alhamisi hii asubuhi, wakazi wa Oisha walikuwa wakielekea maeneo jirani ambayo ni salama, kwa mujibu wa mashahidi.

Shambulio hilo lilitokea muda mfupi baada ya jua kuzama, karibu saa moja usiku (saa za DRC). Jeshi liliingilia kati. Mapigano yalisitishwa saa tatu tu baadaye.

Bakahiku, eneo lililokumbwa na shambulio hilo linapatikana katika mashariki mwa mji wa Oicha, ambao tayari ulikumbwa na shambulio lililosababisha vifo vingi mwishoni mwa mwezi Septemba. Wakati huo, wakaazi wa eneo hilo walilazimika kutoroka makaazi yao.

Wengi walikimbilia katika shule na makanisa magharibi mwa mji huo. Kabla ya shambulio la jana, baadhi ya wakimbizi walikuwa wameanza kurejea makwao, walilazimika tena kukimbilia katika mji wa Ituri na Butembo, kwa mujibu wa serikali katika mji huo.

Wengine asubuhi hii walikuwa bado wakitafuta ndugu zao waliotoweka, huku hofu ikiendelea kutanda katika eneo hilola Bakahiku.

Watu wameshangazwa na jinsi mji wao ulishambuliwa licha ya kuwepo kwa ngome za jeshi.

Hata hivyo kundi la waasi wa Uganda la ADF linahusishwa katika mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.