Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Idadi ya vifo kutokana na Ebola Mashariki mwa DRC yafikia 159

Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, inaendelea kuongezeka.

Timu ya inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC.
Timu ya inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC. REUTERS/Jean Robert N'Kengo
Matangazo ya kibiashara

Hadi siku ya Jumanne idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia ugonjwa wa Ebola ilikuwa imefikia 159, kulingana na ripoti ya tarehe 23 Oktoba 2018 ya shirika la Afya duniani (WHO) .

Wiki mbili zilizopita, WHO ilionya kuwa, kuna hatari ya maambukizi hayo kuendelea kuenea iwapo visa vya maambukizi havutapungua.

Mapema wiki hii Umoja wa Ulaya ulisema unatoa Euro Milioni 7.2 kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msaada wa Umoja wa Ulaya unajumuisha ujuzi wa kiufundi, huduma za angani za kibinadamu, ufadhili wa utafiti na usaidizi wa kibinadamu, ameeleza Christos Stylianides, Kamishna anayehusika na Misaada ya kibinadamu na kukabiliana na Mgogoro katiak umoja wa Ulaya.

Fedha hizi zitasaidia masharika ya afya yanayofanya kazi ya kupambana na maambukizi haya, kuwaajiri watu zaidi kuwasaidia wagonjwa lakini pia kutoa elimu.

Mkoa wa Kivu Kaskazini ndio uanaathiriwa hasa Wilaya ya Beni, na idadi ya watu walipoteza maisha inaendelea kuongezeka kila kukicha.

Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani linasema maambukizi hayo hayajafikia kiwango cha kutisha na kuathiri maeneo mengine duniani.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DRC, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.