Pata taarifa kuu
AFRIKA-HAKI ZA BINADAMU-UTAWALA BORA

Wanaharakati wakutana Gambia kujadili mwenendo wa haki za binadamu barani Afrika

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya Haki za Binadamu barani Afrika unaendelea nchini Gambia ukiwakutanisha wanaharakati na viongozi wa asasi za kiraia kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

Jebra Kambole, Mwanaharakati kutoka Tanzania anayehudhuria Mkutano wa Haki za Binadamu unaofanyika nchini Gambia
Jebra Kambole, Mwanaharakati kutoka Tanzania anayehudhuria Mkutano wa Haki za Binadamu unaofanyika nchini Gambia Youtube
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umeanza jana Oktoba 23 na unatarajiwa kukamilika Novemba 13 ambapo Kabla ya kuanza kwa mkutano huo viongozi wa asasi mbalimbali za kiraia, watunga sera, viongozi wa serikali na wanaharakati za binadamu.

Jebra Kambole ni Wakili kutoka Tanzania anayehudhuria Mkutano huo na ameiambia RFI Kiswahili akiwa Mjini Banjul kwamba wanaharakati wana wasiwasi na mwenendo wa haki za binadamu barani Afrika.

Tumeangazia mwenendo wa haki za kiraia hasa adhabu ya kifo, haki za kisiasa, haki za elimu na jukumu la serikali katika kutoa elimu kwa jamii, tunaona bado kuna changamoto katika mataifa mengi ya Afrika,"

Aidha mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo kuhusu matukio muhimu yanayoyakumba baadhi ya mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayokabiliwa na uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, mwenendo wa kisiasa nchini Burundi na Uganda.

Maazimio ya Mkutano huo yatawasilishwa kwa Kamisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa Afrika ambayo ni mojawapo ya vitengo vya Umoja wa Afrika.

Usikose kusikiliza matangazo yetu ya jioni kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.