Pata taarifa kuu
EU-DRC-EBOLA-AFYA

Umoja wa Ulaya yatenga Euro Milioni 7.2 kukabiliana na Ebola DRC

Umoja wa Ulaya umesema unatoa Euro Milioni 7.2 kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Afisa wa afya nchini DRC akitoa chanjo dhidi ya Ebola kwa mwanamke aliyewasiliana na mwathirika wa Ebola katika eneo la Mangina, Kivu Kaskazini, tarehe 18 Agosti 2018.
Afisa wa afya nchini DRC akitoa chanjo dhidi ya Ebola kwa mwanamke aliyewasiliana na mwathirika wa Ebola katika eneo la Mangina, Kivu Kaskazini, tarehe 18 Agosti 2018. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

"Tume ya Umoja wa Ulaya imetenga euro milioni 7.2 za ziada ili kuongeza uwezo katika kudhibiti virusi vya Ebola, ambavyo bado havijadhibitiwa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,"Umoja wa Ulaya umesema katika taarifa yake.

Jumla ya fedha kwa majibu ya Umoja wa Ulaya kwa mgogoro huu zimefikia sasa milioni 12.83 mwaka 2018.

Msaada wa Umoja wa Ulaya unajumuisha ujuzi wa kiufundi, huduma za angani za kibinadamu, ufadhili wa utafiti na usaidizi wa kibinadamu, ameeleza Christos Stylianides, Kamishna anayehusika na Misaada ya kibinadamu na kukabiliana na Mgogoro katiak umoja wa Ulaya.

Fedha hizi zitasaidia masharika ya afya yanayofanya kazi ya kupambana na maambukizi haya, kuwaajiri watu zaidi kuwasaidia wagonjwa lakini pia kutoa elimu.

Jimbo la Kivu Kaskazini ndilo lililoathiriwa hasa Wilayani Beni, na idadi ya watu walipoteza maisha kutoka na ugonjwa huu imeongezeka na kufikia 153.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Afya Duniani (WHO) ya tarehe 21 Oktoba 2018, watu 155 tayari wamefariki kutoka na virusi vya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.