Pata taarifa kuu
UFARANSA-BURKINA FASO-COTE D'IVOIRE-USHIRIKIANO

Ufaransa yaendelea na jitihada za kuimarisha usalama Burkina Faso na Cote d'Ivoire

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian anafanya ziara rasmi inayolenga kuimarisha usalama pia kuboreshwa kwa mfumo wa elimu nchini Cote d'Ivoire na pia katika nchi jirani ya Burkina Faso.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mataifa haya ya Afrika Magharibi ambayo yameathiriwa na ongezeko la mashambulizi ya kigaidi,yamekabiliwa na matatizo ya elimu kutokana na shule nyingi kulazimishwa kufunga milango, baada ya kuvamiwa na magaidi na hivyo kuwafanya wananfunzi wengi kushindwa kumaliza masomo.

Katika Ziara hii aliyoianza hapo jana jijini Abidjan, waziri Ledrian amekutana na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara majira ya jioni kabla ya kuhudhuria Kongamano la kimataifa linalohusu elimu dhidi ya Ugaidi, project of the International Academy against Terrorism, mradi ambao utaanzishwa mwaka Ujao, maafisa wanaoandamana na waziri huyo wa mambo ya nje wa Ufaransa Wamesema.

Taasisi hiyo iliyoanzishwa na Marais Emmanuel Macron wa Ufaransa Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire kando na Mkutano wa EU na Afrika, itajumuisha shule za kikanda, kituo cha mafunzo cha vitengo vya kiusalama juu ya namna ya kuzuia ugaidi kwenye ukanda huo wa Afrika magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.