Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mgomo katika sekta ya uchukuzi wasitishwa Guinea-Bissau

media Shughuli za uchukuzi zimenza nchini Guinea Bissau AFP/SEYLLOU

Serikali ya Guinea-Bissau na vyama vya uchukuzi wameafikiana Alhamisi wiki hii na kutia saini itifaki ya makubaliano ya kumaliza mgomo uliyozorotesha shughuli nyingi katika nchi hiyo tangu siku ya Jumanne.

aa chache baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo kati ya idara ya uchukuzi, kwa upande wa serikali, na vyama vya uchukuzi, magari ya uchukuzi yameonekana mitaani na kwenye barabara kuu za mji wa Bissau na kuelekea nchi jirani.

Chini ya itifaki ya makubaliano, serikali imejikubalisha kupunguza idadi ya vituo vya ukaguzi ndani ya miezi miwili.

Vyama vya wa uchukuzi vimekuwa vikishtumu kuwepo kwa rvituo vingi vya ukaguzi, huku wakiomba wapewe ufafanuzi zaidi kuhusu majukumu ya kila upande kati ya viongozi mbalimbali wanaohusika na uchukuzi wa watu na mizigo, polisi, kikosi cha ulinzi wa taifa na hasa maafisa wa idara ya uchukuzi wa nchi kavu.

Pia wamekuwa wakilalamikia dhidi ya kodi kuongezwa kiholela na barabara mbovu.

Mbele ya vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa uchukuzi wa ardhini Bamba Banjai amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa na kuomba msamaha kwa matatizo yaliyowakuta wananchi kufutia mgomo huo.

Siku ya Jumatano, kiongozi wa Shirikisho la vyama vya uchukuzi, Bubacar Felix Frederico, alisema kuwa mgomo huo utasitishwa "tu kwa ahadi rasmi ya Waziri Mkuu" Aristides Gomes.

Guinea-Bissau, ambayo ni koloni ya zamani ya Ureno, ni moja ya nchi za mwisho ulimwenguni katika orodha ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo (UNDP) ya nchi zinazojikita na suala la maendeleo ya binadamu.

Kwenye jumla ya kilomita 4,400 za barabara nchini, 10% peke (sawa na kilomita 453) ni barabara za lame.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana