Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kesi ya wakimbizi: DRC yatishia kuichukulia hatua Angola

media Wahamiaji wa DRC wakivuka mpaka kati ya Angola na DRC katika mji wa Kamako tarehe 12 Oktoba 2018. Sosthene KAMBIDI / AFP

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inatishia kuichukulia hatua za Kimataifa nchi ya Angola, kufuatia hatua ya Angola kuwafukuza raia wake wanaokadiriwa kuwa 200,000 kwa madai kuwa walikuwa ni wahamiaji haramu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Leonard She Okitundu amesema, Kinshasa inaitaka Luanda kuchunguza kwa kina aliyeamuru kufukuzwa kwa raia wake na kuchukuliwa hatua, la sivyo itachukua hatua zaidi, kauli aliyoitoa huku akishtumu hatua hiyo.

Serikali ya Angola kwa upande wake imekuwa ikikanusha kuwa iliwafukuza wakimbizi hao kwa lazima kutoka katika mkoa wa Lunda Norte.

Hivi karibuni Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR lilisema lina wasiwasi mkubwa kutokana na wimbi kubwa la idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wanaorejea nyumbani kufuatia hatua ya serikali ya Angola kufukuza wahamiaji.

Raia hao wa DRC walikuwa wakifanya kazi katika machimbo ya madini yasiyo rasmi huko Kaskazini Mashariki mwa Angola, kabla ya kufurushwa na kwamba siku ya Jumatatuwiki Oktoba 15 ilikuwa ni siku ya mwisho ya wageni kupaswa kuondoka nchini humo.

Zaidi ya raia 200,000 wa DRC walikimbilia nchini Angola kwa sababu za kiusalama.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana