Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Chama tawala chaongoza katika uchaguzi wa serikali za mitaa Cote d'Ivoire

media Matokeo ya uchaguzi katika mji wa Tiebissou, Cote d'Ivoire Oktoba 14, 2018. © ISSOUF SANOGO / AFP

Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Cote d'Ivoire uliofanyika siku ya Jumamosi, raia wa nchi hiyo wameanza kutambua majina ya viongozi wao na madiwani wa Majimbo.

Tume ya Uchaguzi nchini Cote d'Ivoire ilikamilisha kutangaza matokeo kamili siku ya Jumanne, Oktoba 16. Chama tawala cha RHDP kinaongoza katika chaguzi zote mbili.

Kiwango cha ushiriki katika uchaguzi wa magavana na madiwani wa Majimbo kilifikia 46.4% na 36.2% katika uchaguzi. Kiwango hicho ni cha juu kidogo lakini kinafanana na kile cha mwaka 2013.

Pamoja na 46% ya kura, chama tawala cha RHDP, kimeshinda wilaya 92, ikiwa ni pamoja na wilaya saba kati ya kumi na tatu katika mji wa Abidjan, ikiwa ni pamoja na Abobo, Yopougon, Kumasi na Treichville. Wagombea wa chama cha RHD wamepata ushindi katika mji wa Bouaké, San Pedro, Korhogo na Bassam ambapo Meya wa chama cha PDCI (Democratic Party of Ivory Coast) anaye maliza muda wake, George Ezaley, anapinga kushindwa na amesema atakata rufaa katika Mahakama Kuu.

Chama cha Henri Konan Bedie, mshirika wa zamani wa chama tawala kwa upande wake kimepata ushindi wa 28 % ya kura katika wilaya 50. Chamahicho kimeshinda katika wilaya ya Cocody mjini Abidjan dhidi ya mpinzani wake na pia Marcory na Plateau. kimeendelea kushikilia ngome yake ya Yamoussoukro.

Kati ya wagombea 389 binafsi, 56 wamechaguliwa. Wamepata 28% ya kura. Kwa upande wa chama cha FPI (Ivorian Popular Front), kimepata ushindi katika wilaya mbili.

Ikumbukwe kwamba uchaguzi ulifutwa katika wilaya ya Port-Bouët huko Abidjan, kwa sababu ya kuchomwa kwa masanduku ya kura. Tume Uhuru ya Uchaguzi ina mwezi mmoja kuandaa uchaguzi mpya.

Katika uchaguzi wa magavana, chama cha RHDP kimeshinda kwa 60% ya kura.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana