Pata taarifa kuu
UGANDA-COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yaanza kutangazwa Cote d'Ivoire

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika nchini Cote D'Ivoire yameanza kutolewa tangu siku ya Jumapili, huku chama cha Upinzani cha PDCI kinachoongozwa na mwanasiasa maarufu nchini Humo Henry Konan Bedie kikijigamba kupata ushindi kwenye uchaguzi huo.

Zoezi la uhesabuji wa kura baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Bouaké, katikati mwa Côte d'Ivoire, Oktoba 13, 2018.
Zoezi la uhesabuji wa kura baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Bouaké, katikati mwa Côte d'Ivoire, Oktoba 13, 2018. Vote workers count ballot papers during Ivory Coast's regional a
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa chama hicho Maurice Kakou Guikahue anasema kumekuwa na uchakachuaji wa kura katika maeneo mengi, na kuongeza kuwa hawatakubali udanganyifu wowote wa kura zao,

Wakati huo huo mchezaji wa zamani wa kimataifa Bonaventure Kalou amechaguliwa meya wa mji wa wakazi karibu 500,000 nchini Cote d' Ivoire.

Bonaventure Kalou aliweza kuichezea klabu ya Paris SG, Auxerre na Feyenoord. Amechaguliwa meya wa mji wa Vavoua, katikati-magharibi mwa Cote d'Ivoire katika uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya Jumamosi.

"Ninafurahishwa sana na maamuzi haya ya wakazi wa mji huu, nimefikia ndoto ya babangu (aliyefariki dunia mwaka wa 2016) ambaye alitaka kuwa meya wa wilaya hii. Nimefuata nyayo zake," Bw Kalou ameliambia shirika la Habari la AFP baada ya ushindi wake kuthibitishwa na mamlaka husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.