Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-EBOLA

Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Ebola yaendelea kuongezeka mashariki mwa DRC

Waziri wa afya nchini DRC dokta Oly Ilunga amesema wamekuwa wakikabiliana na wimbi jipya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa ebola kwenye maeneo ya mipaka ya nchi hiyo na Uganda.

Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC.
Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC. Photo: Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Afya Duniani (WHO), limeonyesha wasi wasi wake kutokana na kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola, eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo idadi ya watu wanaoshukiwa kuambukizwa maradhi hayo imefikia 207, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya tarehe 12 Oktoba 2018.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, katika wiki za hivi karibuni, idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeongezeka huku watu waliokwishapoteza maisha kwa maradhi hayo hadi siku ya Jumamosi wiki iliyopita ikiwa imefikia 130.

Watoto zaidi ya watatu ni miongoni mwa watu waliyopoteza maisha hivi karibuni, kwa mujibu wa maafisa wa Wizara ya afya.

Dk Oly ilunga ni waziri wa afya wa DRC amesema wamekuwa wakishirikiana na nchi jirani na Congo katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kwenye maeneo ya mipakani,

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema imewapa chanjo watu 15,000 katika jimbo la Kivu Kaskazini ili kuepusha maambukizi zaidi.

Wakaazi wa Jimbo la Kivu Kaskazini wametakiwa kuendelea kushirikiana na maafisa wa afya kwa kuwafikisha katika vituo vya afya wale wote wanaoshukwia kuwa na dalili za Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.