Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA-USALAMA

Rais wa zamani wa Nigeria Obasanjo amuunga mkono Atikou Aboubacar

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ametangaza kumuunga mkono katika uchaguzi ujao aliye kuwa makamu wake wa rais wakati huo. Atiku Abubakar tayari ni mpinzani mkuu wa Rais wa anaye maliza muda wake Muhammadu Buhari.

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo.
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo. AFP / Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Msimamo wa Olusegun Obansanjo unaja baada ya miaka ya kadhaa ya mvutano na makamu wake wa zamani Atiku Aboubacar.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Obasanjo alimuandikia barua Rais Buhari akimuomba kutowania kwa muhula wa pili na "kuchukua mapumziko yanayostahili.

Muhammadu Buhari aliteuliwa na chama chake kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais ujao.

Hatua hii ya Obasanjo rais wa zamani wa Nigeria (1999-2007) inakuja wakati ambapo washirika kadhaa wa karibu wa Rais Buhari wameamua kuachana naye.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Wanawake Aisha Alhassan alijiuzulu siku chache baada ya kujiuzulu kwa Kemi Adeosun kama Waziri wa Fedha.

Hata hivyo wanasiasa kadhaa wameamua kuachana na mgombea wa chama tawala cha APC (Congress of Progressives) rais wa sasa wa Nigeria.

Wananchi wa Nigeria watapiga kura kumchagua rais wao mpya mnamo mwezi Februari na Machi 2019, lakini pia magavana na Wabunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.