Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-HAKI

Kesi ya Moise Katumbi yatumwa mbele ya Mahakama ya Katiba

Kesi ya mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Moise Katumbi aliye uhamishoni nje ya nchi imesitishwa na kutumwa mbele ya Mahakama ya Katiba. Moise Katumbi anakabiliwa na mashitaka ya kuajiri mamluki kwa lengo la kuupindua utawala wa Rais Joseph Kabila Kabange.

Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa.
Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya uamuzi huo, kesi ya mpinzani huyo, mshirika wa karibu wa zamani wa rais joseph Kabila, ilisikilizwa mbele ya Mahakama Kuu siku ya Jumatato kwa muda wa saa nne. Hata hivyo watuhumiwa wawili wakuu, ambao ni gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga, Moïse Katumbi, na raia wa Marekani anayefahamika kwa jina la Darryl Lewis hawakuwepo wakati wa kesi hiyo.

Majaji walikataa kuwasikiliza wanasheria wao bila ya wao kuwepo, Jean-Joseph Wa Mulumba, mmoja wa wanasheria hao ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mapema mwezi Agosti, Bw Katumbi, ambaye anaishi uhamishoni nje ya nchi tangu Mei 2016, kwa muda wa siku mbili mfululizo alijaribu kuingia nchini DRC kupitia mpaka wa Kasumbalesa nchini Zambia, ambako alisema hakumpata afisa yeyote upande wa idara ya uhamiaji ya DRC ambaye angeliweza kumuhudumia ili angie kihalali nchini.

Katumbi anasema alitaka kurudi nchini DRC ili kuwasilisha fomu za kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23.

Mshirika wake ulipelekwa kwa waandishi wa habari barua ya Julai 20 ambapo Mheshimiwa Katumbi alimwomba Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo "utoaji wa pasipoti mpya" kuonekana katika mahakama mnamo Oktoba 10 na faili mgombea wa uchaguzi wa rais.

Familia yake inasema Julai 20 Moise Katumbi alituma barua kwa waziri wa mambo ya Nje wa DRC akimuomba aweze kupata pasipoti mpya ili aripoti mahakamani Oktoba 10 na kuwasilisha fomu yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais.

"Serikali imekataa kumpa pasipoti ya kusafiria na haitaki aweze kurejea nchini," familia yake imebaini, huku ikiongeza kwamba ubalozi wa DRC nchini Marekani ulikataa kutoa visa kwa mtuhumiwa mwenzake, raia wa Marekani Darryl Lewis.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijazungumza chochote kuhusiana na madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.