Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 17/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 17/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Soka: PSG-Manchester United na Lyon-Barça watarajia kujitupa uwanjani katika Ligi ya Mabingwa
 • Olympique Lyonnais yatarajia kumenyana na FC Barcelona katika mzunguko wa nane wa Ligi ya Mabingwa
 • Vizibao vya njano: Rais Macron atarajia kufanya mkutano kuhusu mjadala mkubwa Jumatano wiki hii
Afrika

Rais Ramaphosa amteua Waziri mpya wa fedha

media Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa © AFP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua Tito Mboweni kuwa Waziri mpya wa fedha.

Gavana huyo wa zamani wa Benki Kuu, anachukua nafasi ya Nhlanhla Nene aliyejiuzulu siku ya Jumanne baada ya madai kuwa alishirikiana kwa karibu na familia ya kitajiri ya Gupta katika masuala ya kibiashara.

Rais Ramaphosa alikubali kujiuzulu kwake baada ya wiki iliyopita, akiwa mbele ya tume maalum inayochunguza visa vya ufisadi, kukiri uhusiano wake wa kibiashara na familia hiyo.

Familia ya Gupta imekuwa ikihusishwa na rais wa zamani Jacob Zuma, ambaye serikali yake ilituhumiwa kutekwa na familia hiyo.

Waziri huyo wa zamani alisema alikataa kupokea fedha wakati wa uongozi wa rais wa zamani Zuma, wakati serikali yake ilipokuwa inakabiliwa na madai ya ufisadi.

Zuma ambaye amefikishwa Mahakamani kwa madai mbalimbali ya ufisadi, ameendelea kukataa kuhusika na wizi wa fedha za umma akishirikiana na familia hiyo ya tajiri lakini pia alipokuwa Waziri miaka ya tisini.

Ramaphosa amesema serikali yake haitakubali visa vya ufisadi kuendelea.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana