sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Afrika

Maurice Kamto adai ameshinda uchaguzi wa urais Cameroon

media Maurice Kamto katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amedai kuwa ameshinda uchaguzi wa urais, Oktoba 8, 2018 Yaounde. REUTERS/Zohra Bensemra

Siku moja baada ya uchaguzi wa urais nchini Cameroon, wakati matokeo ya awali ya uchaguzi yakiendelea kusubiriwa, Maurice Kamto, mmoja wa wagombea wakuu ametangaza kwamba ameshinda uchaguzi.

Maurice Kamto amesema kuwa ameshinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza. Waziri wa zamani wa Paul Biya ametoa mfano wa mchezo wa soka na kusema ameshinda. Hata hivyo, hakutoa takwimu wala asilimia ya kura alizopata.

"Nilipata nafasi ya kupachika bao na kupata ushindi wa kihistoria kupitia mkwaju wa penalti. Nilipiga mkwaju na nikafunga bao, "Maurice Kamto amesema mbele ya wafuasi wake na waandishi wa habari waliokusanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari.

Maurice Kamto ametangaza kwamba ameshinda uchaguzi huku wafuasi wake wakipiga makofi na kufurahia ushindi huo.

Rais Paul Biya hajazungumza chochote kuhusiana na madai hayo, lakini chama chake kimepuuzia mbali madai ya Maurice Kamto. Kwa upande wa Jacques Fame Ndongo, Waziri wa Elimu ya Juu na Katibu wa Mawasiliano wa chama cha RDPC, chama tawala, amesema madai hayo ni uzushi, na hayana nguvu yoyote.

Akihojiwa na RFI, mgombea wa chama cha SDF, Joshua Osih amesema anastaajabishwa na madai yaMaurice Kamto kwa sababu kwa mujibu wa Bw Osih inachukua muda kwa kukusanya matokeo yote. "Sisi ni chama cha kisiasa cha upinzani ambacho kilikuwa na wawakilishi wengi katika vituo vya kupigia kura. Kwa sasa, ni vigumu kupata asilimia ishirini kutoka vituo vya kupigia 25,000.

Wapiga kura milioni 6.6 walipiga kura Jumapili Oktoba 7 nchini Cameroon kumchagua rais wao mpya. Wagombea nane walishiriki kinyang'anyiro hicho, ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Paul Biya. Uchaguzi ambao ulifanyika katika hali ya utulivu, isipokuwa katika maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza.

Matokeo yanatarajiwa kufahamika, baada ya wiki mbili, katika Uchaguzi ambao rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85, akitarajiwa kushinda na kuendeleza uongozi wake wa miaka 36.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana