Pata taarifa kuu
MISRI-IS-USALAMA

Wanajihadi 52 na askari watatu wauawa Sinai

Wanajihadi Hamsini na mbili na askari watatu wameuawa katika operesheni "dhidi ya magaidi" katika eneo la Sinai, mashariki mwa Misri, ambapo vikosi vya ulinzi vinaendesha vita kabambe dhidi ya kundi la Islamic State (EI), jeshi limetangaza Jumatatu wiki hii.

Kituo cha ukaguzi wa jeshi katika mji wa el-Arish kaskazini mwa eneo la Sinai, Julai 15, 2013, ambapo basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi liliposhambuliwa kwa roketi, na kuua angalau watu 3  na kuwajeruhi wengine 17.
Kituo cha ukaguzi wa jeshi katika mji wa el-Arish kaskazini mwa eneo la Sinai, Julai 15, 2013, ambapo basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi liliposhambuliwa kwa roketi, na kuua angalau watu 3 na kuwajeruhi wengine 17. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya Misri yalizindua Operesheni "Sinai 2018" kwa ombi la Rais Abdel Fattah al-Sissi Februari 9, baada ya shambulizi lililodaiwa na serikali kutekelezwa na kundi la IS, shambulizi ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya 300 watu katika Msikiti wa eneo hilo.

Katika taarifa ya Jumatatu wiki hii, jeshi limetangaza kwamba "limeangamiza magaidi 52 wenye msimamo mkali" wakati wa operesheni mbili tofauti na vikosi vya usalama.

Askari watatu pia walipoteza maisha katika operesheni hizo kwa mujibu wa chanzo hicho ambacho hakikuleza wakati na eneo tukio hilo lilitokea.

Zaidi ya wanajihadi 350 na askari thelathini wameuawa tangu kuzinduliwa operesheni "Sinai 2018", kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Mmoja wa viongozi wa ndani wa EI, Abu Hamza al-Maqdessi, aliangamizwa katika mashambulizi ya kijeshi yaliyoendeshwa na jeshi la Misri huko Sinai, vyanzo vya usalama vimeliambia shirika la Habari la AFP. Hata IS ilitangaza kifo hicho kwenye Telegram.

Tangu kutimuliwa madarakani rais kutoka kundi la Waislamu wenye msimamo mkali nchini Misri Mohamed Morsi, mamia ya polisi na askari lakini pia raia wameuawa katika mashambulizi ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.