Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Ugonjwa wa Ebola wazua hisia tofauti mashariki mwa DRC

Mapambano dhidi ya Ebola yameendelea kukabiliwa na changamoto Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kundi la watu wenye hasira limevamia mazishi ya mama mmoja aliefariki kutokana na Ebola huko Butembo.

Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini.
Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini. REUTERS/Samuel Mambo/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya polisi, gari la kubebea wagonjwa lililokuwa limebeba muili wa mama huyo lilishambuliwa, wafanyakazi wawili wa shirika la Msalaba Mwekundu walijeruhiwa, muili wa mama huyo ukarejeshwa katika kituo kinachotoa tiba ya Ebola.

Baadhi ya watu katika maeneo hayo hawaamini kwamba Ebola ni maradhi badala yake wanaamini kwamba ni maradhi ya kupandikiza. Mkurugenzi mkuu wa Butembo Richard Mbambi Kinwana amesema taarifa potovu imeendelea kuchukuwa nafasi na kutatiza harakati za kupambana na Ebola.

Kuendelea kuripotiwa kwa maradhi hayo pamoja na mauaji ya mara kwa mara katika eneo hilo la mpaka na Uganda kumeendelea kudhoofisha uchumi wa jimbo hilo kutokana na wakulima wengi kushindwa kuendesha shughuli zao za kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.