Pata taarifa kuu
AFRIKA-MELANIA-USHIRIKIANO

Melania Trump aanza ziara yake Afrika

Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump anatarajia kuanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika hasa katika nchi za Ghana, Malawi, Kenya na Misri. Ziara kama hii aliifanya mke wa aliyekuwa rais wa Marekani Michelle Obama nchini Afrika Kusini, China na Cambodia.

Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump (kushoto).
Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump (kushoto). REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Melania Trump ambaye hatashirikiana na mumewe katika ziara hiyo anatarajia kutoa changamoto zinazowakabili watoto.

Hii ni ziara ya kwanza ya Melania Trump, mwana mitindo wa zamani, Mmarekani mwenye asili ya Slovenia kuzuru bara la Afrika.

Ziara ya Melania barani Afrika inalenga kuhamasisha ulinzi wa haki za watoto pamoja na mazingira bora ya utoaji elimu kwenye mataifa atakayotembelea.

Kulingana na maneno ya msemaji wake Stephanie Grisham, ziara ya mke wa tatu wa Rais wa Marekani imetokana na kazi ambazo zinafanywa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika, ambapo amesema maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.

Melania amesema anatarajia ziara yake kwenye mataifa hayo kuwa yenye tija hasa wakati huu ambapo mtoto wa kiafrika ameendelea kukabiliwa na changamoto za kielimu, matumizi ya dawa za kulevya, unyanyasaji, usalama katika matumizi ya mtandao, umasikini na magonjwa, akisema katika karne hii watoto hawapaswi kuwa katika mazingira haya, amesema Stephanie Grisham.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.