Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia yaomba kuondolewa vikwazo vya silaha

Serikali ya Somalia inasema inahitaji silaha zaidi na za kisasa ili kushinda kundi la kigaidi la Al Shabab. Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Ahmed Awad Isse ameitaka Umoja wa Mataifa kuiondolea vikwazo vya kununua silaha.

Vikosi vya usalama vya Somalia vyatoa ulinzi katika eneo kulikotokea milipuko miwili, Mogadishu.
Vikosi vya usalama vya Somalia vyatoa ulinzi katika eneo kulikotokea milipuko miwili, Mogadishu. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Ahmed Awad Isse amebainisha kuwa, japo kuwasafari ya kurejesha amani na utulivu nchini Somalia bado ni ndefu, lakini idiolojia ya genge la kigaidi la al-Shabaab inaendelea kufifia siku baada ya nyingine na kwamba vijana hawajiungi tena na kundi hilo.

Wakati huo huo, Uganda inaitaka Umoja wa Mataifa isifikiri kupunguza msaada wa kifedha nchini Somalia.

Hayo yanajiri wakati hali ya wasiwasi inaendelea kutanda katika miji mbalimbali nchini humo licha ya kuwepo kwa askari wa kikosi cha Amisom.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine wengi kulazimika kuyatoroka makaazi yao.

Somalia ilitumbukia katika mapigano na machafuko ya ndani tangu ilipoondolewa madarakani serikali ya Mohamed Siad Barre mwanzoni mwa muongo wa 1990. Mbali na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabab kuwa tatizo kuu nchini Somalia, nchi hiyo inakabiliwa pia na ukame na baa la njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.