Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Hatari ya maambukizi ya Ebola iko juu sana DRC

Shirika la afya la kimataifa limetangaza kuwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola iko juu sana nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Wataalamu wa afya katika makabiliano na mlipuko wa Ebola jimboni Kivu kaskazini
Wataalamu wa afya katika makabiliano na mlipuko wa Ebola jimboni Kivu kaskazini Photo: Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirika la WHO limetaja njia za usafiri na shughuli za umma zinaongeza hatari ya wananchi kuambukizana huku tathimini ya kimataifa ikiendelea kubaki hatari ndogo.

Taarifa ya WHO imearifu kuwa kitaifa na majimboni nchini humo hatari ya kuambukizana iko juu sana na kushauri majimbo jirani na mataifa kuimarisha tahadhari dhidi ya maradhi hayo.

Aidha WHO imesisitiza kuendelea kushirikiana na mataifa jirani na washirika kuhakikisha mamlaka za afya zinachukua tahadhari na zinakuwa tayari kuchukua hatua.

Mnamo jumanne iliyopita naibu mkurugenzi wa WHO Peter Salama alionya taifa jirani la Uganda kuchukua tahadhari kufuatia tishio la maambukizi mpakani jirani na ziwa Albert.

Kwa mujibu wa takwimu wa shirika la WHO mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vya watu 101 tangu ulipolipuka mnamo mwezi August.

Huu unakuwa mlipuko wa mara ya kumi kutokea nchini DRC tangu mwaka 1976,ambapo hali ya hatari iko juu sana katika jimbo la kaskazini mashariki ambako kunavikundi kadha avinavyomiliki silaha jirani na mpaka wa Uganda Rwanda na Sudani kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.