Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-USHIRIKIANO

Melania Trump aweka wazi ratiba ya ziara yake Afrika

Mke wa rais wa Marekani, Melania Trump hatimaye jana ameweka wazi ratiba ya ziara yake barani Afrika ambapo atatembelea nchi za Ghana, Malawi, Kenya na Misri kuanzia juma lijalo, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kimataifa akiwa peke yake.

Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump Washington, Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump Washington, Marekani. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Melania barani Afrika inalenga kuhamasisha ulinzi wa haki za watoto pamoja na mazingira bora ya utoaji elimu kwenye mataifa atakayotembelea.

Melania amesema haya wakati alipokutana na wake wa marais mbalimbali ambao wanahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, ambapo akaeleza sababu za kuchagua nchi ambazo atatembelea.

Katika taarifa yake Melania amesema ziara yake imetokana na kazi ambazo zinafanywa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika, ambapo amesema maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.

Melania amesema anatarajia ziara yake kwenye mataifa hayo kuwa yenye tija hasa wakati huu ambapo mtoto wa kiafrika ameendelea kukabiliwa na changamoto za kielimu, matumizi ya dawa za kulevya, unyanyasaji, usalama katika matumizi ya mtandao, umasikini na magonjwa, akisema katika karne hii watoto hawapaswi kuwa katika mazingira haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.