Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UN-MANDELA

Sanamu ya Nelson Mandela yazinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Sanamu ya aliyekuwa rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela, imezinduliwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani.

Rais Cyril Ramaphosa anaonyesha sanamu kubwa ya Nelson Mandela kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya serikali na raia wa Afrika Kusini. Sanamu hiyo litawekwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.
Rais Cyril Ramaphosa anaonyesha sanamu kubwa ya Nelson Mandela kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya serikali na raia wa Afrika Kusini. Sanamu hiyo litawekwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York. PresidencyZA/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Hii ndio sanamu pekee katika Makao makuu ya Umoja huo na inaashiria juhudi za Mandela za kuliunganisha dunia na kuhimiza amani wakati alipokuwa hai.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alizindua sanamu hiyo ya kihistoria na kusema inaeleza mchango wa Afrika Kusini katika amani ya dunia.

Sanamu kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria siku moja baada ya rais huyo wa zamani kuzikwa.

Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.

Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.

Mandela alizikwa katika kijiji alikozailiwa cha Qunu, mkoani Cape Mashariki.

Mandela Madiba alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Mandela anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu.

Wakati wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.

Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.