Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Mlipuko katika mgahawa wajeruhi watu 42 kaskazini mwa Japan (serikali za mitaa)
 • Canada yataka kufuta mkataba wa silaha wa dola biloni 15 na Riyadh (Justin Trudeau)
Afrika

Watu 21 wauawa Beni nchini DRC

media Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimamakaribu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmojahuko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018. © AFP

Jeshi la DRC limetoa ripoti mpya ya watu 21 waliouawa na limesema limeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea huko Beni, mashariki mwa nchi hiyo. Mauaji ambayo yamehusishwa kundi la kigaidi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Force (ADF).

"Ofisi ya mashitaka ya kijeshi imefungua uchunguzi kuhusu mashambulizi mabaya yaliyoendeshwa na kundi la Kiislamu la ADF Beni dhidi ya wakaazi wa Beni, na kusababisha vifo vya raia 17 na wanajeshi 4," amesema Kanali Khumbu Ngoma afisa wa mashitaka katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti ya awali iliyotolewa Jumapili jioni ilibaini kwamba watu 18 sawa na raia 14 na askari wanne waliuawa.

Leo Jumatatu asubuhi, shughuli mbalimbali katika mji wa Beni zilizorota katika kuitikia wito wa mashirika ya kiraia kusalia nyumbani. Shule na maduka vimefungwa, huku watu waisalia makwao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana