Pata taarifa kuu
SUDAN-UN-USALAMA

UNAMID kuondoka Sudan ndani ya kipindi cha miaka miwili Sudan

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema kuwa awamu ya tatu na ya mwisho ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur, UNAMID, watakuwa wameondoka kabisa nchini humo katika kipindi cha miaka miwili.

Mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Getty Images/ Robert Caputo
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mwishoni mwa juma, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje Abdel-Ghani al-Nai’m, amesema majimbo manne waliyokuwepo wanajeshi hao utulivu umerejea na kwamba sasa inahifadhi wakimbizi kutoka mataifa mengine.

Licha ya mara kadhaa kuingia katika mvutano na umoja wa Mataifa kuhusu tume yake kwenye jimbo la Darfur, nchi ya Sudan inasisitiza kuendelea kuheshimu mamlaka ya vikosi vilivyoko na itasimamia kuondoka kwao.

Mwezi Juni mwaka 2017 umoja wa Afrika na UN waliamua kupunguza kikosi cha walinda amani wake kwa asilimia 44 ya wafanyakazi wake na asilimia 30 ya polisi ikiwa ni awamu yake ya kwanza ya kuwaondoa kabisa walinda amani hao.

Tume ya umoja wa Mataifa nchini Sudan ni ya pili duniani kutumia bajeti kubwa ya umoja wa Mataifa baada ya ile ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.