Hatua ya kuagizwa kukamatwa kwake imekuja baada ya mwamuziki huyo kutarajiwa kufika Mahakamani siku ya Ijumaa kujibu mashtaka lakini hakuonekana.
Olomide alikuwa nchini Zambia hivi karibuni, na aliondoka licha ya kutakiwa kufka Mahakamani.
Msimamizi wa mwanamuziki huyo nchini Zambia Mark Mumbalama, amesema alikuwa ameimba Mahakama kumpa muda zaidi Olominde kabla ya kuja Mahakamani lakini hakufanikiwa.
Mwanamuziki huyo amekuwa akishtumiwa kwa utovu wa nidhamu kwa kuwashambulia wanahabari na hata wanamuziki wenzake, kama ilivyoshuhudiwa nchini Kenya mwaka 2016.