Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Orodha ya mwisho ya wagombea urais yatangazwa DRC

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congi (CENI) imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea urais nchini wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba.

Mwenyekiti wa Tme huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa, tarehe 5 Novemba 2017 Kinshasa.
Mwenyekiti wa Tme huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa, tarehe 5 Novemba 2017 Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume huru ya Uchaguzi nchini DR Congo Corneille Nangaa amesema kwa sasa hakuna tena kikwazo chochote kinachoweza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa desemba 23 nchini humo.

Bw Nangaa amesema hatua hii inamaanisha kuwa tume hiyo ipo katika hatua ya mwisho kuelekea Uchaguzi huo.

Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe wote wa upinzani na Emmanuel Ramazani Shadary, akiwakilisha chama tawala ni miongoni mwa wagombea 21 watakaowania uchaguzi huo wa urais.

Wanasiasa wawili wakuu wa upinzani, Jean Pierre Bemba, Adolphe Muzito hawatowania nafasi ya urais katika uchaguzi huo, pamoja na Moise Katumbi ambaye hakuwasilisha fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Wakati huo huo Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, imemesema kmekua na ongezeko la vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadam katika Jimbo la Kivu Kaskazini ambako visa 200 vimeripotiwa kuanzia mwezi uliopita.

MONUSCO inasema kuendelea kwa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi, ndio chanzo cha kuendelea kwa visa hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.