Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UPINZANI-UCHAGUZI

DRC: Wanasiasa wa upinzani waendelea kukutana kuelekea Uchaguzi Mkuu

Baada ya mkutano wa viongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo juma lililopita jijini Brussels nchini Ubelgiji,  walikutana nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne na kufanya mashauriano na chama tawala ANC wakiongozwa na Moise Katumbi huku vyama vingine vikiwakilishwa na wajumbe mbalimbali.

Wanasiasa wa upinzani Vital Kamerhe (Kushoto) na  Moise Katumbi, walipokutana jijini Brussels hivi karibuni
Wanasiasa wa upinzani Vital Kamerhe (Kushoto) na Moise Katumbi, walipokutana jijini Brussels hivi karibuni JOHN THYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza chama cha ANC kukutana na upinzani wa DRC baada ya  rais Cyril Ramaphosa kuingia  madarakani ambapo upinzani unaona, kuna mabadiliko kuhusu mtazamo wa Utawala wa nchi hiyo kuhusu mchakato wa Uchaguzi nchini DRC.

Wajumbe hao wa upinzani watakutana pia na viongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, ambayo DRCongo ni mwanachama.

Upinzani unaona kuwa SADC ina mchango mkubwa katika kuishinikiza serikali ya rais Joseph Kabila kuandaa uchaguzi huru wa haki.

Wakati uo huo, Tume ya Uchaguzi CENI, imesema imeanza kupokea vifaa vya kupigia kura kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Miongoni mwa vifaa ambavyo vimewasili kutoka China, ni vibanda vya kupigia kura.

Msemaji wa CENI Jean-Pierre Kalamba, amesema vifaa zaidi vinatarajiwa kuwasili nchini humo vikisafirishwa kwa meli na vitapokelewa na maafisa wake katika Bandari za Matadi, Dar-es-Salam na Mombasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.