Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAJANGA ASILI

Mafuriko yaua watu 100 nchini Nigeria

Nigeria imetangaza hali ya maafa ya kitaifa baada ya mafuriko makubwa ambayo yamesababisha watu watu mia moja kupoteza maisha. Mvua ya kubwa imesababisha mito ya Niger na Benue kujaa, na hivyo mafuriko kuyakumba maeneo wanakoishi watu, mashamba na kuwazuia maelfu ya watu katika nyumba zao.

Nyumba hii ikiwa katika ya maji katika mji wa Lokoja, katika Jimbo la Kogi, Nigeria, Septemba 17, 2018.
Nyumba hii ikiwa katika ya maji katika mji wa Lokoja, katika Jimbo la Kogi, Nigeria, Septemba 17, 2018. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Tumetangaza maafa ya kitaifa katika Majimbo manne: Kogi, Delta, Anambra na Niger," Sani Datti wa taasisi ya kitaifa kwa kukabiliana na Majanga (NEMA) aliliambia shirika la Habari la AFP. Majimbo mengi manane yamewekwa kwenye orodha ya kuangaliwa kwa makini.

"Majimbo yote haya yameathiriwa na mafuriko. Watu wapatao 100 wamepoteza maisha katika majimbo 10," ameongeza.

Kogi na Niger ni katikati mwa Nigeria wakati nchi za Delta na Anambra ziko kusini.

Mji mkuu wa Jimbo la Kogi, Lokoja, unaopatikana kati ya mito miwili umekumbwa na mafuriko makubwa. Kwa mujibu wa NEMA, kiwango cha maji kilikua kinaendelea kuongezeka jana Jumatatu huko Lokoja na kufikia mita 11.06, ikaribia ile ya mafuriko yaliyotokea mwaka 2012. Wakati huo maelfu ya watu waliangamia na karibu milioni mbili walijikuta hawana makaazi katika Majimbo 30 kati ya 36 nchini Nigeria.

Mvua mpya imnatarajiwa kunyesha Jumanne wiki hii, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema siku ya Jumatatu kuwa ameidhinisha kutengwa kwa Naira bilioni tatu (sawa na Dola milioni 8.3, au Euro milioni 7.1) ili kununua vifaa vya matibabu na uokoaji.

Mafuriko karibu na mito yanatokea mara kwa mara nchini Nigeria wakati wa msimu wa mvua kuanzia mwezi Mei hadi mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.