Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Zaidi ya watu 23 wauawa katika machafuko ya kikabila Ethiopia

media Waziri Mkuu wa ethiopia, Abiy Ahmed, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Agosti 25, 2018, tangu achukue mamlaka ya uongozi mnamo mwezi Aprili. REUTERS/Kumera Gemechu

Machafuko ya kikabila yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 23 ndani ya kipindi cha siku mbili zilizopita karibu na mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, katika Jimbo la Oromo, shirika la Habari la serikali la ENA limeripoti.

Mkuu wa polisi katika Jimbo la Oromo, Alemayehu Ejigu, akinukuliwa na ENA, amesema kuwa kundi lililokuwa limejiandaa liliendesha mfululizo wa mauaji na uporaji kuho Burayu, magharibi mwa Addis Ababa, na kuua watu 23 na kusababisha watu 886 kuyatoroka makazi yao.

vikosi vya usalama vilitumwa ili kuzuia hali isiendelei kuzorota zaidi, na watuhumiwa 70 wamekamatwa, chanzo hicho kimesema.

"Waziri mkuu Abiy Ahmed amekemea vikali mauaji hayo na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Fitsum Arega, mkurugeni kwenye ofisi ya Waziri Mkuu.

Umati wa watu wameandamana leo Jumatatu wakipinga machafuko ya wiki hili. Wameshtumu vijana kutoka kabila la Oromo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana