Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wafaransa wawili washtakiwa kwa kupanga mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Congo

media Mji wa Lyon, ambako mahakama ya mji huo imewapata na hatia Wafaransa wawili kwa kupanga mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Congo-Brazzaville . Wikimedia CC BY-SA 4.0/Babsy

Mahakama ya Lyon nchini Ufaransa imewakuta na hatia raia wawili kutoka nchi hiyo wenye umri zaidi ya hamsini kwa kupanga mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Congo-Brazzaville.

Wawili hao, waliozaliwa mnamo mwaka 1961 na 1967, walishtakiwa kwa kosa la "kushirikiana na kundi la wahalifu" na "kumiliki vilipuzi" na wamewekwa chini ya udhibiti wa mahakama. lakini ofisi ya mashitaka imesema haikubaliani na uamuzi huo wa mahakama na imekata rufaa, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Mtu wa tatu, aliyezaliwa mwaka 1962, aliwekwa kama shahidi atakayesaidia kutoa mwanga mbele ya mahakama.

Mahakama inawashtumu kuwa walipanga kuua "katika wiki zijazo" mwanasiasa wa upinzani wa Congo-Brazzaville, anayeishi katika mkoa wa Paris. Mwanasiasa huyo hakutajwa na mahakama, hata majina ya washtumiwa wa mauaji hayo hayakutajwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana