Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Ishirini wapoteza maisha katika ajali ya lori Mali

Watu wasiopungua 20 wamepoteza maisha nchini Mali baada ya gari lililokuwa likiwabeba kuanguka katika mto usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne katika mwa nchi hiyo, serikali imesema, huku ikibaini kwamba tatizo la kiufundi ndio chanzo cha ajali hiyo.

Mtu huyu akikaa kando ya Mto Niger huko Bamako Julai 31, 2018.
Mtu huyu akikaa kando ya Mto Niger huko Bamako Julai 31, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Lori lilikua limebeba abiria ambalo lilikuwa likitokea katika kijiji cha Koué katika wilaya ya kijijini ya Sanna (katika jimbo la Saye) likielekea Macina lilianguka katika mto karibu usiku wa tarehe 10 Septemba, serikali imesema leo Alhamisi katika taarifa yake.

"Watu 63 walinusurika baada ya kuokolewa. Zoezi la ukutafuta miili linaendelea. Kwa mujibu wa ripoti za kwanza za uchuguzi, tatizo la kiufundi linalohusiana na mfumo wa breki ndio chanzo cha ajali hiyo ya kutisha," imesema taarifa hiyo.

Serikali "imewatolea wito wachukuzi kuzingatia sheria za barabara, ambazo zinapiga marufuku usafiri wa watu na mizigo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.