Kwa mujibu wa mashahidi waliohojiwa na wafanyakazi wa MSF, boti mbili ziliondoka pwani ya Libya Septemba 1 asubuhi, na kila boti lilikua limebeba watu 160, kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali.
Kwa mujibu wa MSF, kulikuwa na raia kutoka Sudan, Mali, Nigeria, Cameroon, Ghana, Libya, Algeria na Misri
Kwa mujibu wa mmoja wa manusura akinukuliwa na MSF boti moja lililokua limebeba watu 165 , ikiwa ni pamoja na watoto 20 lilipatwa na tatizo la injini na kuanza kuzama, lakini wachache tu waliweza kuokolewa.
Watu 55 pekee ndio walinusurika. Watoto zaidi ya 20 walifariki, kulingana na chanzo hicho, kilichonukuliwa na MSF.
Waathirika ni pamoja na wanawake wajawazito, watoto, na watoto wachanga, MSF imeongeza.