Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Polisi akamatwa baada ya kufyatua risasi karibu na televisheni ya serikali DRC

Polisi wa DRC amekamatwa baada ya kufyatua risasi mita chache kutoka makao makuu ya Radio na Televisheni ya serikali (RTNC) kaskazini mwa mji wa Kinshasa.

Askari wa FARDC wakipiga doria karibu na makao makuu ya Radio na Televisheni ya serikali (RTNC) Kinshasa tarehe 30 Desemba 2013.
Askari wa FARDC wakipiga doria karibu na makao makuu ya Radio na Televisheni ya serikali (RTNC) Kinshasa tarehe 30 Desemba 2013. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tukiwa ndani ya ofisi zetu, tulisikia milio mingi ya risasi zikifyatuliwa kutoka uwanja unaopatikana mbele ya RTNC. Kulikuwa na makundi mawili, polisi na majambazi wenye silaha," mmoja wa wafanyakazi wa RTNC ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Askari wa kikosi cha ulinzi wa taifa walifika haraka eneo hilo na kuendesha operesheni kubwa, lakini hali ya utulivu imerejea baada ya nusu saa."

"Ilikuwa kama vita," amesema mfanyakazi mwengine wa chombo hicho cha serikali, kinachopatikana karibu na kambi ya kijeshi ya Kokolo, kambi kubwa zaidi ya kijeshi mjini Kinshasa ambako kunahifadhiwa vifaa vingi vya jeshi la DRC.

Akihojiwa na AFP, mkuu wa polisi wa Kinshasa amesema hali hiyo ilisababishwa na "polisi ambaye alifyatua risasi tatu au nne hewani" akijaribu kukabiliana na majambazi wenye silaha waliokua wamekuja kuiba katika eneo la Lingwala mbele ya RTNC ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.