sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Viongozi wa waandamanaji na wa kijeshi …
Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, mkuu wa baraza la kijeshi la Sudan katika Mkutano kwenye kijiji cha Aprag,tarehe juni 22 2019.
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Sita wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Mogadishu

media Hali ya usalama inaendelea kudorora kila kukicha Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Watu wasiopungua sita wameuawa Jumatatu wiki hii katika shambulizi la bomu lililotegwa katika gari mjini Mogadisho, nchini Somalia. Shambulizi ambalo limedaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shabab.

Shambulizi hilo lililotokea Jumatatu wiki hii liliendeshwa katika majengo ya serikali mjini Mogadishu.

Shambulizi hilo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shbab, lenye mafungamano na Al-Qaida, ambalo linajaribu kwa miaka kumi kuangusha serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

"Gari lililokua limejaa vilipuzi liliingizwa ndani ya ofisi ya wilaya ya Hodan huko Mogadishu, bado hatujapata idadi kamili ya watu waliopteza maisha," Mohamed Nur, Mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema.

Kwa mujibu wa mashahidi, ofisi hiyo iliteketea klabisa kwa moto baada ya mlipuko. Jengo jingine la serikali mjini Mogadishu liiliharibiwa vibaya wiki iliyopita katika hali hiyo kama hiyo.

Wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabaab walitimuliwa mjini Mogadishu mnamo mwaka 2011 na kupoteza udhibiti wa miji mingi, lakini bado wapo karibu na mji mkuu wa nchi hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana