Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA-USALAMA

Marshal Haftar: Niko tayari kupigana hadi Tripoli

Kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mapigano huko Tripoli, nchini Libya, kiongozi maarufu mashariki mwa Libya amevunja ukimya wake wakati wa mkutano na wazee wa busara zaidi ya thelathini na viongozi na kutangaza kwamba yuko tayari kudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo.

Marshal Haftar, kiongozi maarufu mashariki mwa Libya, amesema majeshi yake yako tayari kudhibiti mji wa Tripoli (picha ya kumbukumbu).
Marshal Haftar, kiongozi maarufu mashariki mwa Libya, amesema majeshi yake yako tayari kudhibiti mji wa Tripoli (picha ya kumbukumbu). © Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Khalifa Haftar ametuma ujmbe mbalimbali, amnbao ulirushwa hewani moja kwa moja kwenye kituo chake cha televisheni cha Al Hadath. Amepinga katu katu rasimu ya Katiba mpya ambayo inatarajiwa kuidhinishwa na Bunge kabla ya tarehe 10 Septemba, 2018. Lakini alizungumzia has kuhusu Tripoli.

Hii si mara ya kwanza Khalifa Haftar kuonyesha nia yake ya kupigana hadi kwa lengo la kuudhibiti mji wa Tripoli, lakini ni mara ya kwanza anatangaza moja kwa moja na kusisitiza.

Kwa mara kadhaa, alirejelea kauli hiyo akihakikisha kwamba jeshi lake liko tayari na kwamba mji waTripoli utadhibitiwa haraka. Kwa lengo hili, alieleza kwamba ana mawasiliano ya moja kwa moja na vikosi vya miji ya Misrata na Zentan. Bw haftar anayeongoza mashariki mwa Libya amethibitisha kwamba majeshi mji wa Tripoli pia yako tayari kufanya mashambulizi kwa lengo la kuudhibiti mji wa Tripoli.

Mapigano ya hivi karibuni yameanza kubadili taswira ya kuwepo kwa wanamgambo katika mji mkuu. "Hatuwezi kuruhusu Tripoli iwe mikononi mwa waasi na wananchi wa Libya wanapaswa kuishi salama katika mji huu," Khalifa Haftar amesema.

Wachambuzi walio karibu naye wameendelea kupaza sauti ili kuonyesha kwamba Marshal Khalifa Haftar ana haki ya kuwatimua wanamgambo katika mji wa Tripoli kabla ya wezi Novemba, wakati Italia ilitangaza kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Libya.

Italia inataka Uchaguzi Mkuu ufanyike mnamo mwaka 2019 wakati Ufaransai napendekeza Uchaguzi nchini Libya ufanyike kabla ya mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.