Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ufaransa yataka uchaguzi kufanyika Desemba 10 Libya

media François Delattre akisema mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 28 Februari 2017. © REUTERS

Ufaransa kupitia balozi wake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa François Delattre, inapendekeza uchaguzi mkuu nchini Libya ufanyike tarehe 10 Desemba mwaka huu.

"Ni muhimu zaidi kuendeleza mabadiliko ya kidemokrasia nchini Libya," amesema Balozi wa Ufaransa katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya hivi karibuni nchini Libya.

François Delattre amefutilia mbali hoja ya wale ambao wanataka "kuchelewesha mchakato wa uchaguzi kwa kisingizio kwamba hali hairuhusu".

"Adui wa Libya na Walibya ni watu wanaochochea machafuko nchini humo" ambao wananufaika na "uchumi wa nchi hiyo", "biashara haramu" na "uhalifu uliopangwa," amesema Bw Delattre.

Mapigano karibu na Tripoli kati ya makundi ya waasi yameua watu wasiopungua 50 tangu Agosti 27. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) ulitangaza Jumanne wiki hii kwamba makundi hasimu ya waasi yamefikia mkataba makubaliano na yalitia saini mkataba wa kusitisha mapigano lakini hali bado ni tete.

Mapema wiki hii Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, aliishtumu Ufaransa kuchangia katika machafuko yanayoendelea nchini Libya.

Salvini pia amesema "bila shaka, kuna mtu anayechochea (mapigano ya sasa). Hiyo haitoke kwa bahati mbaya. Kwa hofu yangu mimi, mtu kutokana na sababu za kiuchumi, anakubali kuhatarisha usalama wa Afrika ya Kaskazini na, na kupelekea Ulaya kuwa hatarini".

"Nafikiria mtu ambaye alichochea mapigano wakati hakutakiwa kufanya hivyo, kwa mtu anayeweka tarehe ya uchaguzi bila kukutana na washirika, Umoja wa Mataifa na wananchi wa Libya," ameongeza Bw Salvini.

Siku ya Jumatatu, Waziri wa Ulinzi wa Italia, Elisabetta Trenta, pia alisema kuhusu "kuhusika kwa Ufaransa katika kuingilia kati ya kijeshi dhidi ya serikali ya Kanali Gaddafi mwaka 2011.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana