Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-DIPLOMASIA

Ethiopia yafungua Ubalozi wake nchini Eritrea

Ethiopia imefungua tena Ubalozi wake nchini Eritrea, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa mataifa hayo jirani.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akifungua ubalozi wa nchi yake jijini Asmara, Septemba 06 2018
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akifungua ubalozi wa nchi yake jijini Asmara, Septemba 06 2018 fanatelevision
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya rais wa Eritrea Isaias Afwerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mwezi Julai.

Kufunguliwa kwa Ubalozi huu jijini Asmara, kunatazamwa kama kumaliza mvutano wa karibu ya miaka 20 kati ya nchi hizo mbili, hasa kuhusu umiliki wa mpaka kati ya nchi hizo.

Waziri Mkuu Abiy amekuwa nchini Eritrea kwa mara ya pili na kuongoza sherehe za kuongoza Ubalozi huo na kusifia uhusiano mpya kati ya nchi yake na Eritrea.

Mbali na Ubalozi huo, viongozi hao wawili waliungana na rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed, na kutia saini mkataba wa kushirikiana kisiasa, kiuchumi na katika masuala ya kijamii.

Eritrea na Ethiopia ilikuwa nchi moja, kabla ya Eritrea kuamua kujitenga na kuunda nchi yake mwaka 1993.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.